ads

WASANII WAKUTANA NA RAISI MAGUFULI IKULU LEO NIMEKUSOGEZEA YALIOJIRI

Mapema FEB 18 raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DR.JOHN POMBE MAGUFULI alikutana na wasanii mbali mbali wakiwemo bongo movie,bongo fleva na wachekeshaji,Katika hafra hiyo Mheshimiwa raisi akiwa na wasaidizi wake Mh.waziri mkuu na Makamu wa raisi aliweza kutambulishwa baadhi ya wasanii asiowafahamu lakini pia aliongea nao kuhusu kazi zao za sanaa na maslahi ya wasanii,wasanii walitumia nafasi hiyo kuueleza uongozi wa serikali ya awamu ya Tano changamoto wanazozipata na walimuomba aendelee kuwasapoti kwakua sanaa hivi sasa ni ajira na kama serikali itaweka nguvu zake hakika tatizo la ajira litapungua kwa kiasi kikubwa.
Mheshimiwa raisi aliwaahidi kuwa atahakikisha serikali yake inathamini kazi zao lakini pia nao wajitume na wafanye kazi kwa bidii na kuwasihi wafanye kazi kwa ushirikiano kwakua umoja ndio siri ya mafanikio.
WASANII WAKUTANA NA RAISI MAGUFULI IKULU LEO NIMEKUSOGEZEA YALIOJIRI WASANII WAKUTANA NA RAISI MAGUFULI IKULU LEO NIMEKUSOGEZEA YALIOJIRI Reviewed by ENDBOY on 08:09:00 Rating: 5

No comments:

OUR LOGO

Copyright @2015 EdNel TZ. Theme images by caracterdesign. Powered by Blogger.